Serikali imekanusha madai kuwa inapanga kuwapiga kalamu walimu walioajiriwa na wazazi na bodi za usimamizi wa shule za upili.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mkurugenzi wa Elimu Kaunti ya Mombasa Abdikadir Kike, amesema kuwa shule za serikali nchini hazina walimu wa kutosha hivyo basi kuwepo wa walimu hao ni jambo muhimu katika kuimarisha sekta ya elimu nchini.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Kike aliwahimiza walimu hao kuwajibika katika kazi yao, na kuonya kuwa watakao zembea kazini watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha, alisema kuwa serikali imepiga marufuku masomo ya ziada wakati wa likizo, na kuwashauri wazazi kuhakikisha kuwa watoto wao wanajisomea wakiwa nyumbani.

“Ningependa kuwaambia wakaazi wa Kaunti ya Mombasa kuwa serikali imepiga marufuku masomo ya ziada wakati wa likizo na pia wazazi wahakikishe watoto wao wanasoma wakiwa nyumbani,” alisema Kike.

Mkurugenzi huyo aidha aliaahidi kuzuru shule mbalimbali kuwahimiza walimu kutia bidii katika kuwaelimisha wanafunzi.