Wito umetolewa kwa serikali kuhakikisha walimu wa kutosha wanaajiriwa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Katika mahojiano, mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kivumbini Stellah Muluvi alisema kuwa tatizo kuu katika sekta ya elimu ni ukosefu wa walimu wa kutosha. "Baadhi ya shule zina walimu wengi ilhali zingine zina upungufu wa walimu,"Muluvi alisema.

Wakati huo huo, Muluvi aliongeza kuwa serikali inafaa kuhakikisha kwamba inaainisha idadi ya walimu katika baadhi ya shule.

Hata hivyo, anasema kuwa ikizingatiwa shule ya Sekondari ya Kivumbini ni mpya chini ya ufadhili wa CDF, anatumai serikali itahakikisha kuwa inatuma walimu ili kuimarisha elimu katika jamii.

Mwalimu huyo alikuwa akizungumza afisini mwake wakati wa mahojiano ya kipekee.