Serikali imeanza zoezi ya kufunga taasisi zote ambazo zinatoa mafunzo za uuguzi na hazijasajiliwa na bodi ya kutoa mafunzo hayo.
Akiongea katika warsha ya walimu wakuu wa taasisi za kutoa mafunzo ya uuguzi siku ya Jumatatu, waziri wa afya nchini Cleophas Mailu amesema kuwa taasisi hizo zinazotoa mafunzo kinyume na sheria huenda zinatoa mafunzo bandia kwa wakufunzi wake.
Aidha waziri huyo pia amesema kuwa kufikia mwezi wa Juni, kaunti zote nchini zitakua zimepokea vifaa vya matibabu kutoka kwa serikali kuu huku akisema kuwa tayari kaunti 24 zimeshapokea vifaa hivyo.
Vile vile, Mailu amesema kuwa wizara ya afya ikishirikiana na wafadhili wengine wana mpango wa kusaidia katika ujenzi wa mahosipitali katika kaunti ambazo hazina hospitali za kisasa.