Waziri wa kilimo na uvuvi nchini Willy Bett amesema kuwa ni lazima kuwe na uwazi kwenye uuzaji wa majani chai pamoja na wakulima wanaokuza zao hilo kufaidika.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza kwenye kongamano la kamati ya bunge kuhusu ukulima na washikadau kwenye sekta ya ukulima katika makao makuu ya chama cha wauzaji wa majani chai cha EATTA, (East African Tea Trade Association) huko Mombasa, Bett alisema kuwa licha ya zao hilo kuletae nchi ya Kenya fedha za kigeni kwa kiwango kikubwa, wakulima wanaokuza zao hilo huwa hawapati faida.

Bett alisema kuwa ni wadau wachache katika sekta hiyo ambao hunufaika kutokana na mauzo ya zao hilo.

Aidha, waziri huyo alisema kuwa wizara yake iko mbioni kuhakisha kuwa zao hilo linaimarika.

Alisema kuwa wataweka mikakati kuhakisha kuwa wanatafutia azao hilo soko katika bara la Uropa na Asia.