Serikali kuu imetoa ahadi ya kununua meli itakayogharimu shilingi bilioni 3.5 ili kuimarisha vita dhidi ya uvuvi haramu nchini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza alipohudhuria mkutano wa kamati ya bunge kuhusu kilimo na uvuvi siku ya Jumatano katika hoteli ya Whitesands, Kaunti ya Mombasa, Waziri wa Kilimo na Uvuvi Willy Bett, alisema kuwa wataalam wamedokeza kuwa serikali hupoteza takriban shilingi bilioni kumi kupitia wavuvi haramu ambao huepuka kulipa ushuru.

Aidha, Bett alisema kuwa kulingana na ripoti kutoka kwa wizara hiyo, imebainika kuwa licha ya kanda ya Pwani kuwa eneo kubwa zaidi linalofanya bishara ya uvuvi, eneo hlio huchangia asilimia tano pekee ya mapato kutoka biashara ya samaki nchini.

Alisema kuwa hali hiyo imetokana na hatua ya wavuvi haramu wanaoendesha biashara yao katika eneo hilo, kuwauza samaki hao nje ya nchi.