Serikali imesema kuwa kuna umuhimu wa upanuzi wa shule za humu nchini ili kukidhi idadi kubwa ya wanafunzi. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza Jumamosi katika shule ya Mary Mother of Mercy Girls kaunti ya Nakuru, Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa kuna mikakati ya kuhakikisha kwamba miundo inaimarishwa shuleni. 

"Na mimi kila mara nawaambia tuweze kupanua madarasa na shule zetu ili tuweze kukidhi idadi kubwa ya wanafunzi humu nchini ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu," alisema Rais.

Wakati huo huo, alitumia fursa hiyo kushtumu upinzani kuhusiana na kitendo cha juma lilopita ambapo wabunge kadhaa walitatiza hotuba ya Rais. 

"Tafadhali siasa za ukabila na matusi hatutaki katika taifa hili, iwapo unakosoa, fanya hivyo kwa njia mwafaka," alisema Rais. 

Na akizungumza katika hafla hiyo, katibu katika wizara ya Elimu Dr Belio Kipsang alisema kuwa wanafanya mazungumzo na viongozi wa kidini kuhusiana na mtaala mpya wa elimu humu nchini.

Picha: Rais Uhuru Kenyatta katika shule ya Mary Mother of Mercy Girls Nakuru hapo Jumamosi. Ametoa wito wa kupanuliwa shule ili kukidhi idadi kubwa ya wanafunzi.PMambili/Hivisasa.com