Kamishna wa Mombasa Nelson Marwa amewakosoa maafisa wa mamlaka ya ushuru katika kaunti ya Mombasa, wale wa shirika la ukadiriaji wa ubora wa bidhaa nchini KEBS kwa kushindwa kukabiliana na bidhaa za magendo katika kaunti hiyo.
Hii ni baada ya kunaswa kwa magunia ya nafaka ukiwemo mchele ambao siku ya Jumatano katika mabohari ya nafaka eneo la Changamwe mjini Mombasa unaominika kuwa kuwekwa upya kwenye magunia ili kuuzwa.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Alhamis, Marwa alisema huenda maafisa hao wanashirikiana na wamiliki wa mabohari hayo ambao hukwepa kulipa ushuru na akahoji kwamba kama afisa tawala atajitahidi kuukabili ufisadi.
Marwa amesema kwamba ataongoza oparesheni sawa na hizo katika mabohari na maghala mengine ya uhifadhi wa vyakula na bidhaa nyinginezo ili kufanya oparesheni hizo.
“Serikali imejitolea kuhakikisha kuwa ufisadi katika eneo la pwani unakabiliwa kikamilifu ili kusitisha unyanyasaji wa mali ya umma na uingizaji bidhaa nchini kinyume cha sheria,” Marwa alisema.