Serikali ya kitaifa ina mipango ya kutoa hati miliki millioni 4.2 kabla ya uchaguzi mkuu wa 2017. Waziri wa ardhi Jacob Kaimenyi amedokeza.
Prof Kaimenyi alisema serikali tayari ishatengeneza hati miliki milioni 2.4 ili kutimiza ahadi zake wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wa kutoa hati miliki millioni tatu.
"Kwa mwaka ujao serikali ya Jubilee itapeana milioni 1.2 ya hati miliki zilizobaki. Haya ni katika mchakato wa kutimiza yale Rais Uhuru Kenyatta aliahidi Wakenya na sasa timu 17 ziko mashinani ili kuhakikisha utengenezaji wa hati miliki zaidi,"alisema Prof Kaimenyi.
Waziri huyo wa Ardhi alikuwa akiongea katika kaunti ya Kitui ambapo alitoa hati miliki 24,000 kwa wakazi wa Mwingi Kaskazini, Mwingi Kati na Mwingi magharibi.
Waziri Kaimenyi alikuwa ameandana na katibu mkuu wake na vile vile maofisa wengine wa ardhi.
Mbunge wa Mwingi Kaskazini John Munuve na mwenzake wa Mwingi magharibi walikuwa katika hafla hiyo ya kupatiana hati miliki iliyofanyika katika bustani ya Musila Garden.