Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kitaifa imetakiwa kuzisaidia zile za kaunti katika kutekeleza majukumu ya ugatuzi.

Gavana wa kaunti ya Kwale ambae pia ni naibu mwenyekiti wa baraza la magavana  Salim Mvurya, amesema kuwa kuna baadhi ya majukumu ambayo hayajabainika kuwa yako chini ya uongozi gani.

Mvurya ametaja swala la maji ambalo limegatuliwa lakini bado kuna bodi za mikoa  zinazotekeleza majukumu yanayofaa kutekelezwa na kaunti akiashiria shida ya kukatwa kwa maji mwezi uliopita na bodi ya kusambaza maji ukanda wa Pwani.

Mvurya aliyasema haya kwenye ufunguzi wa hafla ya mawaziri 460 kutoka kwa kaunti zote nchini  mjini Mombasa ikiwa ni matayarisho ya kongamano la kitaifa la kila mwaka la ugatuzi ambalo mwaka huu litaandaliwa katika kaunti ya Meru mwezi wa Aprili.