Serikali ya kitaifa imelaumiwa kwa kutoheshimu sheria ambazo zinahitaji wananchi wengine kufuata nchini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya serikali kuchukua mda mrefu kutoheshimu agizo la mahakama la kumrejeshea mbunge wa kitutu Masaba Timothy Bosire walinzi wake ambao alinyanganywa kwa majuma mawili yaliyopita.

Kulingana na Bosire, serikali imeonekana kutoheshimu serikali na kuilaumu pakubwa huku akiomba serikali kuwa kielelezo kizuri kwa wananchi haswa kwa kuheshimu sheria

Mbunge huyo wa kitutu Masaba alipata afueni siku ya Jumatano baada ya kurejeshewa ulinzi wake baada ya kufika mahakamani na kushtaki waziri wa usalama Nchini Joseph Nkaissery, mkuu wa sheria Githu Muigai kwa kumnyanganya ulinzi wake bila kuelezwa sabababu.

Jaji wa mahakama ya Nairobi Isaac Lenaola alitoa makataa ya masaa kwa waziri Nkaissery kurejeshea Bosire ulinzi wake au ashtakiwe kwa kutoheshimu sheria, jambo ambalo lilisababisha Bosire kurejeshewa ulinzi wake siku ya Jumatano kabla ya saa nane mchana jinsi iliagizwa na mahakama.