Kiongozi wa vijana katika chuo kikuu cha Kisii John Otao ameomba serikali kuongeza kiwango cha pesa ya Uwezo Fund ili kuinua maisha ya vijana nchini.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea na mwandishi huyu Otao alisema kuwa pesa za Uwezo Funds zimewasaidia vijana wengi ambao wengi wao walikuwa wamekosa tumaini.

“Naomba wabunge wetu kushinikiza serikali kuongeza pesa za uwezo Fund ili kuendelea kunufaisha vijana,” alisema Otao.

Aidha, aliwaomba vijana kijiunga  katika vikundi ili waweze kunufaika na pesa hizo.

Otao alisema kuwa pesa hizo zitasaidia vijana kujiinua kimaisha.

Kwingineko amewaomba vijana kutotumiwa na wanasiasa kwa njia ya kuwapotosha,na kuwaomba kuijihusisha na miradi ya maendeleo.

“Ni jambo la kuhuzunisha kuona kuwa wanasiasa hutumia vijana kujiendeleza kisiasa bila kujali maslahi yao,” alisema Otao.

Otao pia ameomba serikali kuimarisha usalama katika vyuo vyote nchini.

“Ni vizuri serikali ihakikishie wanafunzi usalama wao iliwaweze kusoma bila uoga,” aliongeza Otao.