Afisa msimamizi wa bima ya matibabu katika kaunti ya Kisii amesema serikali kuu itawalipia malipo ya bima watu waliozeeka 8,778 ambao wamesajiliwa katika kaunti hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubia wanahabari mjini Kisii, afisa huyo kwa jina Bernard Masiita alisema serikali inahitaji kutoa usaidizi kwa watu hao ambao wamezeeka kwa kutokuwa na uwezo wa kulipa pesa zinazohitajika wanapougua ili kupata huduma za matibabu.

“Kufikia sasa tumesajili watu 8,778 ambao ni wazee na ajuza ambao wataanza kulipiwa bima ya NHIF kupitia serikali ya kitaifa maaana idadi kubwa yao hawajiwezi,” alikiri Masiita.

“Kile kimebaki ni kuwapiga picha watu hao ili tuwatengenezee kadi zile za NHIF ambazo wanatumia na kusajiliwa kwa mahospitali ambayo watahudumiwa kimatibabu wanapougua,” aliongezea Masiita.

Kwa upande wa wazee hao ambao tulifanikiwa kuhoji walipongeza serikali kwa kuanzisha mradi huo ambao utawanufaisha wengi kimatibabu na kuomba serikali kuendelea kutoa usaidizi huo kila mara .