Serikali itawekeza zaidi katika miradi ya afya pamoja na ujenzi wa barabara katika maeneo ya mashinani, ili kupiga jeki huduma za afya pamoja na usafiri.

Share news tips with us here at Hivisasa

Haya ni kwa mujibu wa Naibu Rais William Ruto aliyekuwa akiongea katika eneo la Sirikwa wilayani Kuresoi, baada ya kukagua miradi kadhaa ya maendeleo, na alisema uwepo wa umoja miongoni mwa viongozi nchini bila misukosuko ya kisiasa kutachangia ukuaji wa uchumi kupitia utalii na uwekezaji.

Amesema mikakati imewekwa ili kutakaza eneo bunge la Kuresoi kaskazini kama wilaya mpya, huku akiahidi kwamba serikali imekadiria mpango huo.

Rutto amesema serikali itatengeneza kilomita mia tatu za lami katika kaunti ya Nakuru, ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa, mawasiliano na biashara.

Rutto ameongeza kusema serikali kuu pamoja na zile za kaunti zitatumia kima cha shilingi milioni mia saba katika huduma za afya kwa kujengwa kwa hospitali mbili za rufaa katika kila kaunti ili kuwaepushia wananchi mzigo wa kusafiri hadi miji mikubwa ili kutafuta huduma za afya.

Wakati huo huo naibu rais amewataka wawakilishi wa wadi wa jimbo la Nakuru kutumia njia mbadala za kutatua mizozo inayoshuhudiwa katika bunge hilo badala ya kupigana vita na kuzua taharuki.