Serikali ya Kaunti ya Kisumu imekamilisha mradi wa ujenzi wa mtandao wa wi-fi utakawahudumia wakaazi wa kaunti hiyo bila Malipo yeyote.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Katika mahojiano na wanahabari afisini mwake, naibu mkurugenzi wa habari, mawasiliano na tecknologia (ICT) katika serikali ya kaunti ya Kisumu Tom Ogolla, amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kuzinduliwa rasmi katika baadhi ya maeneo jijini Kisumu ifikiapo mwishoni mwa mwezi huu.

Ogolla amesema mradi huo ulichelewa kutokana na baadhi ya changamoto kutoka kwa wafanyibiashara, ambao hawakutaka majumba yao yatumiwe katika kuweka vifaa kusaidia kuimarisha mtandao huo.

Ogolla amesema mradi huo vile vile utahakikisha kuwa wakaazi wote wa kaunti hiyo wanapata huduma ya mtandao wa bure, kama njia mojawapo ya kuboresha sekta ya mwasiliano.

Mradi huo unatarajiwa kuwanufaisha wengi wa wakaazi wa mji huo, haswa wanafunzi ambao wanategemea mtandao kwa maswala ya masomo yao.