Serikali kuu kwa ushirikiano na shirika la Seacom mjini Mombasa inalenga kuzindua mradi wa utanzawazi yaani Swahili Pot mjini humo ili kuwawezesha vijana kutumia fursa hiyo katika kufanyikisha malengo yao ya teknolojia.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Waziri wa teknolojia na mawasiliano nchini Joe Mucheru alisema kuwa tayari Mega byte 100 zimetolewa na shirika la Seacom zenye uwezo wa kusambaza utandawazi kwa kasi zaidi kwani tayari shirika la Makavani na Urathi nchini wametenga maeneo ya ukumbi wa Swahili Culture kuwa eneo rasmi.

Mucheru alisema kuwa utanzawazi huo utatumika bila vijana kutozwa ada yoyote ili kuwahakikisha kuwa wanajishughulisha vyema na maswala ya talanta, teknolojia na utalii ili wanavutia watalii wengi eneo la Mombasa na Pwani kwa jumla.

"Tunapanga kuzindua utandawazi wa kiteknolojia na hatua hiyo itawawezesha vijana wengi kutumia teknolojia katika kutekeleza malengo yao ya kufanikisha ndoto zao hasa katika maswala ya talanta, utalii na teknolojia," alisema Mucheru siku ya Jumanne baada ya kutembelea shirika la makavazi na urathi maeneo ya Swahili Culture mjini Mombasa.

Wakati uo huo, amewaonya vijana kutotumia mtandao huo vibaya na badala yake kuteleza wanayoazima katika siku za usoni huku akiwahakikisha kuwepo na usalama dhabiti kwa maafisa wa usalama watapeyana ulinzi kwa wakaazi wataohudhuria eneo hilo na kaunti nzima ya Mombasa.