Naibu Rais William Ruto amesema serikali iliyoko mamlakani ya Jubilee ndio serikali ya kipekee ambayo imejitolea kupambana na ufisadi nchini kuliko serikali za hapo awali.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ruto alisema serikali ya Jubilee imerudisha kiwango fulani cha pesa zilizoporwa huku akisema zaidi ya kesi 300 za ufisadi zingali zinaendelea katika mahakama.

Haya aliyasema siku ya Jumanne jioni katika hafla ya kujibu maswali kutoka kwa wakenya kuhusu yale serikali imefanya tangu iingie mamlakani hafla ambayo ilipeperushwa moja kwa moja kupitia baadhi ya runinga nchini.

Ruto alitetea serikali ya Jubilee dhidi ya tuhuma za kushindwa kukomeza ufisadi kwa kusema Jubilee ndio serikali ambayo imejitolea kupambana na ufisadi kwa kiwango kikubwa

“Serikali ya Jubilee itaendelea kupambana na ufisadi na penye tumefikia, serikali hii ndio ambayo imefanya mengi kupambana na ufisadi kuliko zingine,” alisema Ruto.

Wakati huo huo, Ruto alimtetea Rais Kenyatta dhidi ya matamshi mbayo aliyoyatoa alipokuwa kwa ziara nje ya nchi ambapo alisema Kenya ni stadi katika kutekeleza ufisadi.

Rais Kenyatta anatarajiwa kutoa hotuba yake hapo kesho siku ya alhamisi kuhusu serikali ya Jubilee