Mkuu wa Idara ya Mazingira katika Kaunti ya Mombasa Tendai Lewa ametoa hakikisho kwa wakaazi wa Mombasa hasusan wanaoishi katika mitaa ya mabanda kuwa serikali ya kaunti imeweka mikakati ya kupambana na mafuriko ya mvua.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza siku ya Jumatatu mjini Mombasa Lewa alisema kuwa serikali ya kaunti itahakikisha kuwa wakaazi hawaathiriki kutokana na majanga kama vile mafuriko.

Hii ni baada ya wakaazi wa mitaa duni katika Kaunti ya Mombasa kusema kuwa wanahofia huenda wakaathirika endapo mvua iliyoanza kunyesha itazidi.

Wakaazi hao walisema kuwa wanahisi kuwa bado serikali ya Mombasa haijafanya juhudi zifaazo kukabiliana na majanga yaliyowakumba katika misimu ya mvua iliyopita.

Tayari mitaa kadhaa na pia barabara katika maeneo mbalimbali ya Mombasa, zimefurika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku ya Jumapili.