Wakaazi wa kaunti ya Kisii wamepongeza serikali ya kaunti hiyo kwa kuimarisha usalama ndani na nje ya  wa uwanja wa Gusii wakati wa sherehe za siku kuu ya Madaraka hiyo jana.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakizungumza na mwandishi huyu wa habari mnamo siku ya jumanne katika mji wa kisii wengi wa wakaazi hao walipongeza hatua serikali ya kaunti hiyo ilichukua kwa kuhakikisha usalama umeimarishwa katika uwanja wa michezo wa Gusii stadium.

“Tunapongeza serikali ya kaunti hii jinsi iliimarisha usalama katika uwanja wa Gusii wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 52 tangu nchi ya Kenya ijinyakulie Uhuru,” alihoji Elijah Nyakundi, mkaazi na mwanabiashara wa viatu katika mji wa Kisii.

Aidha, wakaazi hao walisema ni heri serikali za ugatunzi zipokezwe sekta ya usalama ilii kupunguza visa vya uhalifu ambavyo vinaendelea kushuhudiwa katika sehemu mbalimbal za nchi.

“Usalama ukiwa chini ya ugatuzi hatutasikia mashambulizi kutokea hapa nchini lakini masuala ya usalama ukisalia kuwa chini ya serikali ya kitaifa, basi hatutakuwa na njia ya kupunguza mashambulizi chini,” alisema Meshack Makori mkaazi mwingine alitaja.

“Lakini usalama ukiwa chini ya ugatuzi basi kila kitu kitakuwa sawa hata sisi wananchi hatutakuwa na woga maana serikali ya kaunti ndio inajua mipaka iliyoko karibu na kaunti husika,” aliongeza Makori.

Wakaazi hao walimpongeza gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae kwa kuhakikisha kuwa usalama uliimarishwa kwa uwanja wa Gusii jana wakati maisha ya watu wengi walihudhuria sherehe hiyo.