Mwakilishi mteule katika Bunge la Kaunti ya Nakuru Emmah Mbugua ametoa wito kwa serikali kutenga fedha za kutosha ili kukuza talanta mbalimbali miongoni mwa watu wanoishi na ulemavu katika kaunti hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea na mwandishi huyu siku ya Jumatano, Bi Mbugua ambaye anawakilisha watu wanaoishi na ulemavu kwenye bunge la Kaunti ya Nakuru alisema kuwa baadhi ya walemavu katika kaunti hiyo wana talanta kama vile ya uchoraji, uimbaji, kuigiza miongoni mwa talata zingine.

Bi Mbugua alisema kuwa vipaji hivyo vitakuzwa tu iwapo serekali itatenga fedha za kutosha kuhakikisha kuwa kila mlemavu aliye na talata ameshirikishwa vikamilifu.

Aliongeza kuwa walemavu hupata asilimia kumi na tano tu ya fedha za kufadhili michezo ya walemavu, kutoka kwa shilingi nusu milioni ambazo zimetengewa michezo katika kila wadi.

Mwakilishi huyo alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ni kidogo kuitaka serekali ya kaunti kuwatengea fedha zaidi.

Vile vile, Mbugua aliomba serikali kuwapa watu wanaoishi na ulemavu nafasi ya kutoa burudani wakati wa sherehe mbalimbali za kitaifa ili kuwapa motisha katika kukuza talanta zao.