Serikali ya Kaunti ya Mombasa imetakiwa kuwa mstari wa mbele katika kutunza Soko la Kongowea.

Share news tips with us here at Hivisasa

Katibu mkuu wa Wizara ya ardhi, ujenzi na maendeleo, Aida Munano, ameitaka serikali ya kaunti kutunza jengo jipya la kibiashara katika soko hilo pindi litakapo wasilishwa kwako baada ya ujenzi kukamilika.

Munano ameitaka kaunti kuhakikisha kuwa hali ya juu ya usafi inadumishwa katika soko hilo, ili wafanyabaishara kuendeleza biashara zao katika mazingira shwari.

Akizungumza siku ya Jumatano katika ziara yake ya kulikagua jengo hilo kuhakikisha limejengwa kwa njia ifaayo, Munano alimtaka mwanakandarasi wa ujenzi huo kuweka juhudi katika kukamilisha jengo hilo ili lizunduliwe kwa wakati ufao.

Katibu huyo alisema kuwa ujenzi huo ni hatua mojawapo ya serikali kuafikia ruwaza ya 2030, huku akiongeza kuwa jengo hilo liligharimu zaidi ya milioni mia tatu.