Serikali ya kaunti ya Mombasa imeitetea uamuzi wa bunge la kaunti hiyo ya kununua zaidi ya ekari930 katika shamba la Waitiki kwa niaba ya wakaazi wa eneo hilo kama halali kwa kuwa serikali hiyo inayoongozwa na gavana Hassan Joho ilipata idhini kutoka kwa bunge la kaunti hilo.
Msemaji mkuu wa serikali ya kaunti hiyo Richard Chacha siku ya Jumamosi alisema kuwa serikali hiyo haikukaidi sheria yoyote katika uamuzi huo bali ilifanya hivyo ili kunufaisha wakaazi maskini ambao hawawezi kulipa pesa walizotakikana kulipa
Baadhi ya viongozi katika kaunti hiyo akiwemo seneta Hassan Omar, mbunge wa Likoni Masoud Mwahima na mbunge wa Nyali Hezron Awiti walikuwa wamekashifu uamuzi huo wakisema kuwa Gavana Joho alikuwa akitafuta umaruufu wa kisiasa kutumia maswala ya ardhi ya Waitiki na bali hakuwa na nia njema.