Serikali ya kaunti ya Nakuru imetoa madawa ya shilingi milioni 71 katika hospitali kwenye kaunti ndogo za eneo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Dawa hizo zilitolewa siku ya Alhamisi katika kaunti ndogo ya Kuresoi.

Akitoa dawa hizo, gavana Kinuthia Mbugua alisema kuwa serikali ya inajizatiti kuhakikisha kuwa sekta ya afya inafadhiliwa vilivyo.

“Serikali yangu itahakikisha wananchi wanapata huduma boraili kuinua maisha yake,” Kinuthia alisema.

Kinuthia vile vile alisema serikali yake itaendelea kutoa huduma kupitia kaunti ndogo katika mfumo unaofahamika kama ‘outreach programme’.