Serikali ya Mombasa kupitia kwa Idara ya Fedha katika kaunti hiyo imezindua bajeti yake ya mwaka wa 2016/2017.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza katika kikao na wakaazi wa Mombasa siku ya Jumanne, Mkuu wa Idara ya Afya katika Kaunti ya Mombasa Bi Nuru Khamisi alisema kuwa baada ya kushauriana na washikadau tofauti, serikali ya Kaunti ya Mombasa iliamua kutengeneza bajeti ya shilingi bilioni 9.9.

“Katika bajeti hiyo ya mwaka 2016/2017 takriban shilingi bilioni sita zinatarajiwa kutoka kwa serikali kuu huku shilingi bilioni 3.9 zikitarajiwa kutoka kwa ushuru unaokusanywa kutoka kwa Kaunti ya Mombasa,” alisema Bi Khamisi.

Hata hivyo, idara hiyo imesema kuwa itatilia manani maoni ya wakaazi ambao walihusishwa na kufanya marekebisho zitakazopendekezwa.