Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae ameomba yeyote mwenye shamba la kuuza kati ya hekari tano na kumi katikla eneo lililoko karibu na mji wa Kisii kuwauzia liwe la kutupa taka.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea katika mji wa Kisii siku ya Jumapili, Gavana Ongwae alisema Serikali yake inatafuta shamba la kutupa taka ambazo hukusanywa katika mji huo.

Hii ni baada ya taka kutapaka katika eneo la Nyambera mahala ambapo taka hizo umekuwa ukiwekwa kwa muda mrefu.

“Yeyote auzaye shamba lililoko karibu na mji huu wa Kisii awajulishe Maafisa wa Kaunti ili tupate shamba la kutupa taka ambzo zimekuwa kero kwetu kwa muda mrefu,” alisema Ongwae

Wakati uo huo Ongwae aliomba wakaazi wa Kaunti hiyo kushirikiana naye kuwafukuza wanyakuzi wa mashamba katika eneo hilo ili Serikali yake ikabidhiwe mashamba yao ambayo yalinyakuliwa.

“Kama sio wanyakuzi hawa walijinyakulia mashamba ya Serikali, tayari tungekuwa na kiwanja cha kuweka taka,” aliongezea Ongwae.

Kwa upande mwingine, wakaazi wa Kisii walifurahishwa na ombi la Gavana huyo kushiirikiana naye ili wanyakuzi wa mashamba ya Serikali katika enero hilo watambulike na warudishe kwa wamiliki halali.

“Gavana wetu ameonekana kutukumbuka kwani kama sisi wakaazi tupo tayari kushirikiana naye ili wanaomiliki mashamba ya serikali kwa njia isiyo halali watimuliwe mara moja,” alihoji Cecilia Gesare mkaazi ambaye pia ni mfanyibiashara katika mji huo.