Serikali ya kitaifa imehimizwa kuingilia kati kusuluhisha mzozo ulioko mpakani Keroka kati ya kaunti ya Kisii na ile ya Nyamira.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wito huo umetolewa baada ya madai kuwa serikali hizo mbili za kaunti zimeshindwa kusuluhisha mzozo huo wa mpaka jambo ambalo limegeuka na kuwa vita kali kati ya wakaazi wa Nyamira na wale wa Kisii.

Kati ya Kaunti hizo mbili kila kaunti inahitaji kumiliki soko la Keroka huku mpaka wa kutenganisha kaunti hizo ukikosa kuafikia mpaka sasa.

Akizungumza siku ya Jumanne mwenyekiti wa Wakfu wa Jomo Kenyatta (JKF) Walter Nyambati ameomba serikali kuu kuingilia kati kuleta suluhu halisi kabla ya watu wengi kujeruhiwa .

“Magavana wa Kisii na Nyamira wameshindwa kusuluhisha changamoto iliyoko katika mji wa Keroka naomba serikali ya kitaifa kuingilia kati kuleta utulivu kabla ya wengi kujeruhiwa,” alisema Nyambati.

Katika mji huo wa Keroka vita vikali vilishuhudiwa hivi majuzi huku wengi wakijeruhiwa na baadhi yao kupelekwa hospitali kwa matibabu.