Mwanamke mmoja kutoka kaunti ya Garissa amepata zawadi yenye thamana ya juu kwa kujishughulisha na vita dhidi ya ugaidi.
Asha Hassan, mwenye umri wa miaka 24 alipata tuzo hilo la “Emerging Young Leaders award 2016” siku ya Alhamisi wiki iliopita kule Washington DC, baada ya kuorodheshwa na wenzake kumi kutoka ulimwengu mzima. Alizawadiwa na waziri wa diplomasia na maswala ya umma, Richard Stengel ambaye alimsifu Asha kwa ujasiri wake katika vita hivyo.
“Asha aliunda na kuongoza kundi la kuhimiza mazungumzo na maridhiano baina ya ukoo za Garissa huku akiwa na lengo ya kuwaleta wasichana wadogo wasomali pamoja na kuwahimiza waweze kuleta mabadiliko katika vita dhidi ya ugaidi, tunamzawadi wa kazi hii nzuri,” alisema Stengel.
Asha alisema kuwa alishughulika sana katika kumwingiza nduguye mdogo katika kundi la magaidi ya Al-Shabaab, kisha alipogundua maovu yanayotekelezwa na kundi hilo aliamua kuanzisha kampeni dhidi ya ugaidi nchini.
Naibu kiongozi wa misheni Marekani, David Gacheru alisema kuwa Kenya inashirikiana na Marekani katika vita dhidi ya ugaidi.
“Tunatumai ushirikiano wetu na Marekani itatusaidia hivi karibuni kusuluhisha janga la ugaidi ambayo inakumba Kenya,” alisema Gacheru.