Serikali ya kaunti ya Mombasa imelaumiwa kwa kulivunja na kuharibu sanamu la kipekee la Mamba ambalo ni kivutio kikubwa cha utalii eneo la Nyali.
Mwanahistoria Sheihk Abdurahim Bakathir, ameonyeshwa kusikitishwa kwake kwa kuvunjwa sanamu hilo ambalo amelitaja kuwa kivutio cha utalii na rasilimali za kale.
Bakathir amesisitiza kuwa serikali ingelihamisha sanamu hilo badala ya kuliharibu.
Aidha, ameongeza kuwa kuharibiwa kwa sanamu hilo kutadimiza pia jina maarufu la shamba la Mamba Village ambalo umarufu wake ulitokana na kuweko kwa sanamu hilo la kipeke.
Sanamu hiyo ambayo iliundwa miaka 41 iliyopita, ilikuwa kivutio kikuu cha watalii ambao walikuwa na mazoea ya kupiga picha kando ya sanamu hiyo iliyochongwa na wataalam kutoka nchi ya Israeli.
Inasemekana sanamu hilo lilivunjwa ili kutoa nafasi kwa upanuzi wa barabara.