Serikali ya kaunti ya Nakuru imejitolea kukabiliana na maswala ya unyakuzi wa ardhi kwenye kaunti.
Huo ni usemi wa naibu gavana wa kaunti ya Nakuru Joseph Ruto aliyekuwa akizungumza kwenye shughuli ya kukabidhi zaidi ya waendeshaji 200 wa bodaboda jaketi zenye kiakisi ( reflector jackets) Ijumaa tarehe 18 Desemba.
Ni sisitizo ambalo ametoa huku akiangazia kisa cha unyakuzi wa ardhi ya ekari 3 katika eneo la Soilo anayosema inayomilikiwa na serikali ya kaunti ya Nakuru.
Wakati huo huo, naibu gavana huyo wa kaunti ya Nakuru Joseph Ruto amewata wote kuzingatia sheria za barabarani na haswaa waendeshaji wa bodaboda ambao wengi wao wamehisishwa na matukio ya uvunjaji wa sheria hizo , hatua ambayo huwapelekea kuhatarisha maisha yao na maisha ya wale wanotumia barabara.
Pia, Ruto amewahimiza waendeshaji wa bodaboda kwenye kaunti ya Nakuru kuiga mfano wa waendeshaji bodaboda wengine kwenye sehemu mbalimbali za Dunia kama vile wale wa Rwanda ambao amesema wanatii sheria za barabarani pakubwa na isitoshe, kuna hatua kali zinzochukuliwa dhidi ya wanaokiuka sheria hizo nchini humo.
Katika shughuli hiyo iliyofanywa kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Nakuru na Malka ya usafiri na usalama wa barabarani NTSA pamoja na kampuni ya magari ya CMC Motors, mwenyekiti wa Sacco ya wanabodaboda katika kanda ya bonde ya kati (Nakuru Central Rift Bodaboda Sacco) Stanley Musyoka amepongeza serikali ya kaunti ya Nakuru pamoja na mamlaka ya NTSA na kampuni hiyo ya CMC Motors kwa kuwaunga mkono akisma hatua hiyo itasaidia pakubwa katika kuboresha usalama wa waendeshaji bodaboda pamoja na wengine.
Kwa upande wake, meneja wa halmashauri ya NTSA kaunti ya Nakuru Rosemary Oduor aliyehudhuria shughuli hiyo aliwashauri waendeshaji wa bodaboda kutoendesha bodaboda hizo kwa mwendo wa kasi , ambapo pia aliangazia swala la wanabodaboda hayo kuwa na leseni na pia kutowabeba abiria kupita kiasi na pia kuzingatia usalama wa abiria.
Alisiitiza kuhusiana na usalama wa waendeshaji bodaboda hao akisema usalama huo unafaa kuzingatiwa kila wakati .
Kando na kuangazia maswala hayo, naibu gavana Ruto pia aliwahimiza wanachama wa Jubilee kuunga mkono muungano wao mpya wa Jubilee party uliobuniwa hivi maajuzi na ambao utatumiwa na Rais Uhuru Kenyatta kuomba kura ya urais kwenye uchaguzi mkuu ujao wa tarehe 8 Agosti 2017.
Kulingana naye, chama hicho cha Jubilee party kina maono ambayo anadai yatawaleta watu wote pamoja.