Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amesema kuwa serikali yake imeweka mikakati kuhakikisha kwamba wahudumu wa afya 230 walioajiriwa na serikali yake hivi maajuzi wametumwa kuhudumu kwenye zahanati mbalimbali.
Akihutubu Borabu, Nyagarama alisema kuwa amemwagiza katibu wa afya kwenye kaunti hiyo kuwatuma wahudumu hao wa afya hadi kwenye zahanati zote katika kaunti hiyo ili kuwahudumia wagonjwa.
Gavana Nyagarama aliongeza kuwa atahakikisha kuwa angalau zahanati zote za eneo hilo zimepokea wahudumu wawili kwa kila moja ili kusaidia kushughulikia mahitaji ya wananchi kwa urahisi.
"Jukumu la serikali yangu ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu nao na ndio maana tunataka kuona kwamba kila zahanati ina angalau wahudumu wawili wa afya,” Nyagarama alisema.