Waziri wa elimu kaunti ya Nyamira Jones Omwenga amejitokeza kusema kwamba serikali ya kaunti imefanikisha kuezekwa kwa nyaya za mawasiliano ardhini almaarufu 'Fibre optic cables'.
Kwenye mahojiano siku ya Jumanne Omanwa alisema kuwa tayari serikali ya kaunti hiyo imefanikisha kuezeka nyaya za mawasiliano mjini Nyamira ili kufanikisha mawasiliano.
"Ni furaha kutaja wazi kwamba tayari tumefanikisha kuezeka nyaya za ardhini kutoka eneo la Konate-Nyamira mjini kwa kuwa tunataka kufanikisha mawasiliano miongoni mwa wananchi kwa urahisi," alisema Omwenga.
Omwenga aidha aliongeza kusema kuwa serikali ya kaunti hiyo imejenga madarasa ishirini kwenye wadi zote eneo hilo ili kufanikisha masomo ya wanafunzi walio na chini ya miaka mitano.
"Miaka mitatu baada ya serikali za kaunti kuanzishwa serikali ya kaunti hii imefanikiwa kujenga madarasa ishirini kwenye maeneo wodi yote 20 hapa Nyamira kwa minajili ya kufanikisha elimu ya watoto wetu wa chini ya miaka mitano," aliongezea Omwenga.