Serikali ya kitaifa imeaswa kutenga pesa kwa wakulima wa majani chai katika sehemu za Kisii jinsi ilivyotengea pesa kwa wakulima wa Miraa katika sehemu za Meru ili kuinua na kuimarisha kilimo chao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kulingana na mwenyekiti wa chama cha Kenya National Congress, Atati Kengere, iwapo serikali ya Jubilee inajali maslahi ya wakulima wa majani chai sharti iwatengee kiwango fulani cha pesa ili kilimo hicho kiimarike katika eneo hilo.

Kengere alisema kuwa kilimo cha majani chai kimekuwa miongoni mwa kilimo ambacho hakifanyi vyema katika sekta ya biashara na kuomba serikali ya kitaifa kujaribu kuinua kilimo hicho.

“Kilimo cha majani chai katika sehemu za Kisii hakifanyi vyema kimapato, ninaomba serikali kuu kutenga pesa kwa wakulima wa mumea huo katika sehemu za Kisii ili kilimo hicho kiinuke jinsi ilivyofanyika katika sehemu za Meru,” alikiri Kengere.

Pia Kengere aliomba serikali kuu kuhakikisha viwanda vya majani chai katika eneo la Sombogo na eneo la Matunwa vimeanza kujengwa ili kunufaisha wakulima kutokana na hasara wanayopata wakati majani chai yao hukaa kwa vituo vya ununuzi bila kuchukuliwa viwandani kwa wakati unaofaa.