Afisa mkuu mtendaji wa Tume ya KNATCOM Dr Evangeline Njoka katika hafla ya awali. Picha/ unescochairr.uonbi.ac.ke

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wizara ya Elimu imehimizwa kujumisha lugha za kitamaduni katika mtaala wa masomo ili kukuza utamaduni na thurathi za jamii tofauti tofauti.Kwenye kikao na wanahabari mjini Mombasa, afisa mkuu mtendaji wa Tume ya KNATCOM Dr Evangeline Njoka alisema kuwa kutokuwa na mafunzo ya kitamaduni shuleni kumechangia idadi kubwa ya vijana humu nchini kutofahamu mila na tamaduni zao, hatua aliyoitaja kupelekea wengi wao kujiunga na makundi ya kihalifu na hata utumizi wa mihadarati.Njoka alihoji kuwa kuna haja ya jamii humu nchini kushirikiana vyema na mashirika yanayoshughulika na maswala hayo ili kuhakikisha kuwa mila na tamaduni zinadumishwa vyema.Vile vile, alisema kuwa kama tume watahakikisha vijana wanapewa mwelekeo bora wa kufahamu mila na tamaduni zao ili waweze kujinasua na maswala ya kihalifu.Aidha, Njoka amewahimiza Wakenya kutumia tamaduni zao vyema katika njia ya kuwaunganisha na kuwaleta pamoja.“Tusitumie tamaduni kuleta migawanyiko ya kikabila hususan kipindi hiki cha kampeni na uchaguzi mkuu,” alisema Njoka.Wakati huo huo, Njoka ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuendeleza kampeni zao vyema ili kuunganisha jamii kupitia tamaduni zao, njia moja ya kudumisha hali ya amani wakati wa uchaguzi mkuu.