Sekta ya utalii itaimarika zaidi iwapo barabara na miundo msingi zitaboreshwa zaidi ili kuhakikisha kuwa shughuli za uchukuzi na zinafanyika vyema.
Mkurugenzi wa Chama cha Watalii nchini yaani 'Kenya -Coast Tourist Asssociation', Millicent Adhiambo amesema kuwa kuimarishwa kwa mipango hiyo kutavutia wawekezaji wengi Mombasa na eneo zima la Pwani.
Akiongea katika hafla ya mjini Mombasa siku ya Jumatano, Adhiambo amesema kuwa iwapo serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya kutoka uwanjwa wa ndege wa Moi mjini Mombasa, ujenzi wa reli ya kisiasa na vivukio vya abiria mjini Mombasa, basi sekta ya utalii itaimarika.
Adhiambo amesema kwamba miundo msingi duni katika eneo la Pwani imeathiri pakubwa sekta ya utalii kutokana na kucheleweshwa kwa watalii kutoka eneo moja hadi lingine huku akitaja kukithiri kwa misongamano ya mara kwa mara katika kivuko cha feri kunazidi kudidimiza sekta hiyo.
"Kufuatia kuwepo kwa muundo msingi duni mjini Mombasa na maeneo mengine ya Pwani kumechangia pakubwa kudidimia kwa sekta ya utalii lakini iwapo serikali itakamilisha miradi yake kwa wakati basi sekta hiyo itarejea hali yake ya hapo awali," alisema Adhiambo.
Hata hivyo, ameitaka wizara ya serikali nchini kushirikiana na wadau wa sekta hiyo pamoja na wawekezaji nchini kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inaimarika zaidi na kurejelea hali yake ya hapo awali na kuinua uchumi wa nchini unaimarika.
Picha: Mkurugenzi wa chama cha Watalii nchini yaani Kenya -Coast Tourist Asssociation Millicent Adhiambo kwenye mkutano wa wavuvi. Amesema kuwa kuimarishwa kwa mipango hiyo kutavutia wawekezaji wengi Mombasa na eneo zima la Pwani.