Serikali Kuu imeombwa kutenga fedha zaidi katika bajeti yake ya mwaka kugharamikia karo za wanafunzi wa taasisi za kiufundi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kwenye mkutano na wanahabari mjini Mombasa siku ya Alhamisi, Naibu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mombasa Padri Wilbard Lagho alisema kuwa serikali inafaa kuliangazia swala hilo kwa kina ili kuwasaidia wananfunzi wasiojiweza na kufanikisha masomo yao.

Lagho alisema kuwa iwapo serikali italizingatia swala hilo, basi idadi kubwa ya wanafunzi wanaoshindwa kusonga mbele kielimu watafaidika sambamba na kuwatenga na uhalifu.

Kiongozi huyo wa dini aliwahimiza vijana wasiojiweza hasa mayatima kujiunga na chuo cha kiufundi kinachofadhiliwa na Kanisa Katoliki la Mombasa, ili kutimiza ndoto zao maishani.

"Tunaiomba serikali kutenga fedha zaidi zitakazogharamia masomo ya wanafunzi wasiojiweza katika taasisi za kiufundi, ili kuwawezesha kufanikisha ndoto zao. Hatua hiyo itawasaidia vijana kujiepusha na kujiunga na makundi ya kihalifu,” alisema Padri Lagho.