Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kitaifa na zile za kaunti zimeombwa kutenga fedha kwa wafanyibiashara wanawake ili kuwawezesha kujiendeleza kibiashara.

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Alhamisi mjini Kisii, akina mama hao ambao ni wafanyibiashara wakiongozwa na Mary Rosana waliomba serikali hizo kubuni hazina na kutenga pesa kwa akina mama ambao hufanya biashara ili kuwawezesha kupokea mikopo itakayo wainua kibiashara.

“Ikiwa serikali hizi zetu zinahitaji uchumi kuinuka zaidi, sharti akina mama wapewe pesa za kutosha kwa kutengewa pesa zao ili kuzitumia kufanyia biashara,” alisema Rosana.

Mwishoni mwa juma lililopita, Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae alitangaza kuwa atahakikisha wakazi wa kaunti hiyo wananufaika kibiashara chini ya uongozi wake.

Akina mama hao walimtaka Ongwae kutekeleza ahadi yake kwa kuwatengea wanawake hazina yao.