Mbunge wa Kuresoi Kaskazini Moses Cheboi amezitaka serikali za kaunti katika maeneo kame kuwekeza katika sekta ya kilimo na unyunyizaji maji mashamba ili kukabiliana na uhaba wa chakula nchini.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Cheboi, ambaye amependekaza wananchi katika maeneo kame kukuza mimea inayostahamili kiangazi, amesema huenda sehemu mbali mbali nchini zikakabiliwa na baa la njaa baada ya zao la mahindi kukosa kunawiri katika eneo la Bonde la Ufa.

Amesema ni sharti serikali za kaunti ziweke mikakati dhabiti ili kudumisha usalama wa chakula na kupambana na kero la upungufu wa chakula. 

Mbunge huyo amesema ukosefu wa mvua ya kutosha katika miaka ya hivi majuzi kumesababisha kuharibika kwa mimea mashambani, huku wakulima wakiendelea kukadiria hasara kubwa.

Aamesema ugonjwa wa mahindi ulipunguza zao hilo kwa kiwango kikubwa, akitaka utafiti mwafaka pamoja na ushauri kutolewa kwa wakulima ili kuwapunguzia hasara msimu ujao.

Cheboi alikua akiongea baada ya kutoa hundi za kufadhili miradi ya maendeleo (CDF) katika eneo bunge lake, amesema uhaba wa chakula ni tatizo kwa ukuaji wa uchumi.

Amesema mpango wa serikali ni kupunguza bei ya mbegu pamoja na pembejeo na pia kununua mahindi kwa bei nzuri, shughuli ambayo inatekelezwa na bodi ya kitaifa ya mazao na nafaka nchini.