Mkurugenzi mkuu wa Shirika linalowasaidia watoto na wanawake wanaokumbwa na mateso ya kisaikolojia la ‘Solidarity with women in Distress' Ruth Lewa amesema kuwa visa vya watoto kufariki katika vinaongezeka.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatato, Lewa amesema kwamba kama wanaharakati wa maswala ya haki za watoto na wanawake, tukio hilo huwatia uchungu mwingi na lazima serikali za kaunti ziibuke na mikakati ya kuzuia hali hiyo.
Lewa amesema kwamba matukio ya watoto wa kike kupachikwa mimba wakiwa katika umri mdogo vimekithiri mno na ni lazima serikali za kaunti eneo zima la pwani zishirikiane na wadau wa maswala ya elimu na haki za watoto ili kuidhibiti hali hiyo.
Afisa huyo wa maswala ya haki za watoto na wanawake nchini amekariri kwamba serikali za kaunti na ile kuu wamesahau majukumu yao katika kuyashughulikia maswala ya watoto na wanawake hali iliyopelekea dhuluma nyingi kwa watu hao.
"Tunaiomba serikali kuu na zile za kaunti kuhakikisha kuwa zinawajibikia makujumu yao ya kuwalinda watoto na wanawake ili kuepukana na maafa ya watoto wachache wakati wa wanawake wanapojifungua," alisema Lewa.
Picha: Mwanamke mjamzito. Wadau wa maswala ya haki za watoto na wanawake wanashinikiza serikali kuu na za kuanti kuwalinda vyema wanawake na watoto kuepukana na maafa.