Serikali imekosolewa kwa kusitisha shughuli ya kuwaajiri walimu wapya.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kivumbini katika Kaunti ya Nakuru, Bi Stellah Muluvi amesema kuwa itakua jambo la busara iwapo serikali itaajiri walimu zaidi au kuanisha waliopo.

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumanne, mwalimu mkuu huyo alisema kuwa baadhi ya shule zina walimu wengi ilhali idadi katika baadhi ya shule ni kidogo mno.

"Ni jambo la kusikitisha kwamba baadhi ya shule zina walimu wengi ilhali kwingine hamna walimu wa kutosha. Hakuna usawa hata kidogo,” alisema Muluvi.

Aidha, Bi Muluvi alisema kuwa serikali kupitia Tume ya kuwaajiri walimu TSC, inafaa kuangazia swala hilo ili kuwe na usawa.

Shule ya sekondari ya Kivumbini ilijengwa kwa ufadhili wa hazina ya eneo bunge la Nakuru mjini Mashariki.