Share news tips with us here at Hivisasa

Kasisi wa kanisa la katoliki ya Kisii ilioyoko mjini Kisii, ambaye pia ni mwanakamati wa tume ya kupambana na madawa ya kulevya katika mkoa wa Nyanza, Lawrence Nyaanga, amedai kuwa machifu na maafisa wa polisi hurusu uzaaji wa pombe kuendelea kufanywa katika kaunti ya Kisii kwa kuchukua hongo kutoka kwa wagema hao.

Akizungumza siku ya Jumatatu na waandishi wa habari katika mji wa Kisii, kasisi huyo alisema uzaaji wa pombe umeongezeka pakubwa kufuatia machifu na manaibu wao pamoja na maafisa wa utawala kuruhusu uzaaji huo kuendelea.

Alisema kuwa jambo hilo limemkera sana na kuomba kamishena wa kaunti ya Kisii Chege Mwangi kuingilia kati.

“Uzaaji wa pombe ni janga ambalo limegharimu maisha ya watu wengi katika kaunti hii ya Kisii. Watu hawapaswi kuwa wanapoteza maisha yao kwasababu ya pombe haramu haswa katika lokesheni ya Kiong’anyo,” alisema Nyaanga.

Hii ni baada ya lita 800 za pombe haramu inayojulikana kama chang’aa kumwagwa siku ya Jumapili katika lokesheni ya Kiong’anyo.

Nyaanga alisema watu wengi wataendelea kupoteza maisha yao ikiwa swala hilo halitaangaliwa kikamilifu.

Kasisi huyo ameomba serikali kuingilia kati maana vijana wa umri mdogo ambao hawajaoa wanapoteza maisha bila kuwa na familia katika jamii ya mkisii.