Vingozi wa shirika liliso la kiserikali la Ecumenical Centre for Peace and Justice (ECJP) kwenye tawi la Kisumu wametaka Serikali kutolegeza kamba kwenye vita dhidi ya uhalifu na ufisadi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Viongozi hao ambao walikutana Jumatano kwenye ofisi hiyo ya tawi la Kisumu kupeana mafunzo kwa kundi la kinamama linalo hamazisha jamii eneo hilo kuhusu haki za kibinadamu ilioko katika eneo la Daraja Mbili Maseno, walitaka Serikali kuwachukulia hatua za kisheria wote waliopatikana na kashfa za ufisadi kwenye Wizara mbali mbali za Serikali.

Walisema kuwa mtindo unaoendelea nchini wa viongozi kurushiana maneo makali wakati makosa yametokea na baadaye hali kuishia nyongo bila suluhu, haitazaa matunda yoyote kwa raia wa nchi hii.

Akizungumza kuhusu swala hilo baada ya kikao, Mwenyekiti wa ECJP Charles Ogeto alitaka vyombo vya sheria kuwajibika vikamilifu wakati walio na makosa wanapofikishwa mbele yao.

“Kwa taifa hili kupata maendeleo na ustawi kamili, sharti sheria kufanya kazi bila mapendeleo ya rangi au kabila. Taifa lisilozingatia sheria kwenye maamuzi yake huanguka na kuletea raia wake matatizo,” alionya Ogeto.

Viongozi hao walisifia hatua ya Mahakama ya Naivasha kumchukulia hatua kali za kisheria Mwenyekiti wa chama cha ODM tawi la Nakuru, Peter Ole Osono ambaye alifikishwa Mahakamani jana (Jumatano) akikabiliwa na mashtaka kadhaa likiwemo kuwafyatulia risasi Waandishi wa Habari mnamo Mei 22, 2015 kule Oljorai Kaunti ya Nakuru.

Walisema kuwa hali hiyo inawatia wanyonge moyo baada ya wakenya wengi kubakia na dhana kwamba sheria za Kenya zinafanya kazi kwa raia wa chini pekee huku zikikaliwa na wakuu.