Wakazi wa Limuru wamearifiwa na serikali ya kaunti kuwa takataka kutoka nyumba binafsi inastahili kuokotwa na makampuni ya kibinafsi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Afisa mkuu anayewakilisha serikali ya kaunti huko Limuru, Justa Mwangi alisema haya wakati alitembelewa afisini mwake na wenye nyumba za kukodisha huko Limuru.

Watu hawa walikuwa na malalamishi kuwa kwa wiki kadhaa wafanyakazi wa kaunti hawajafika katika nyumba zao na kuokota takataka ambayo sasa ilikuwa hatari kuletea wapangaji wao magonjwa.

Mary Wawira alisema, “Takataka imekuwa ikiongezeka tu na nzi wanapata raha huku wapangaji wakigadhabishwa na hali hiyo na ndivyo maana tukafika hapa kujua shida iko wapi.”

Naye Mwangi aliwaambia kuwa chini ya uongozi mpya wa serikali za kaunti, wafanyakazi wa kaunti watakuwa sasa wakiokota takataka katika nyumba za biashara peke yake.fallen trees

“Lazima kama mwenye nyumba utafute kampuni ya kibinafsi ambayo huokota takataka na mkubaliane kiasi cha pesa utalipa ili wakuwe wanaokota takataka,” alisema Mwangi.

Baadhi za nyumba za wapangaji huko Limuru zimeongezwa pesa kwa kiasi cha Sh100-150 ili kulipa kampuni ambazo zinaokota takataka. Ni hali mpya ya maisha chini ya serikali ya kaunti.

Kawaida, kulikuwa na gari ambalo lilikuwa linazunguka kote Limuru na wafanyakazi wa kaunti kuchukua takataka na kuzibeba na kuzitupa mbali na maakazi ya watu.

Takataka huwa kizungumkuti kwa nchi nyingi haswa takataka ya kielektroniki kama simu, runinga na redio pamoja na taka ya makaratasi ya plastiki.