Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mkurugenzi wa vyuo vya taaluma mbalimbali nchini TIVET, Bashir Mursal, ametoa wito kwa serikali kuhakikisha kila shule ya msingi inapata kufaidika na mradi wa vipakatalishi ili kuboresha viwango vya elimu nchini.

Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Moi tawi la Mombasa siku ya Jumatano, wakati wa hafla ya kufunza walimu watakaotoa mafunzo ya vipakatalishi katika shule za msingi, Mursal aliwataka wakuu wa vyuo vikuu vya Moi na Jomo Kenyatta waliopewa kandarasi ya mradi huo kuzingatia usawa wakati wa shughuli hiyo.

“Huu ni wakati mwafaka wa kukumbatia teknolojia mpya ili kuimarisha viwango vya masomo nchini katika shule zetu za msingi. Hata hivyo, waku wa vyuo hivi wanahitaji kuepukana na ufisadi na ubaguzi wakati wa kutoa huduma hiyo ili kufanikisha mradi huu,” alisema Mursal.

Profesa wa Chuo kikuu cha Moi David Tuigong kwa upande wake aliwataka wadau mbalimbali kushirikiana ili kufanikisha mradi huo na kuendeleza mapato nchini kupitia elimu bora.