Wanaharakati wa kupambana na dawa za kulevya kanda ya Pwani wameitaka serikali kulichunguza vyema tatizo la utumizi wa mihadarati shuleni.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakiongozwa na Famau Mohamed Famau, wanaharakati hao walisema kuwa wamesikitishwa na jinsi mihadarati inavyopenya shuleni, licha ya kuweko na walimu na hata walinzi.

Famau alisema idadi kubwa ya vijana wanaojiingiza katika utumizi wa mihadarati wamekosa kupata usaidizi katika vituo vya urekebishaji tabia, kutokana na ongezeko la waathiriwa sawia na upungufu wa vifaa kwenye vituo hivyo.

Aidha, alisema kuwa janga hilo linahitaji suluhu la haraka kwani hata vijana wenye umri wa miaka 10 pia wameathirika na dawa hizo.

Famau aliyataja maeneo ya Shella, Maweni, Kisumu Ndongo, Muyeye na Mtangani, kama baadhi ya maeneo yenye idadi kubwa ya walanguzi wa mihadarati, huku akisema kwamba serikali imelegeza kamba dhidi ya vita vya mihadarati eneo zima la Pwani.