Mkurugenzi wa Muungano wa Wahudumu wa Mahoteli katika eneo la Pwani amesema kuwa sekta ya utalii huenda ikaimarika maradufu nchini bila kutegemea watalii kutoka mataifa mengine, iwapo utalii wa ndani utaazingatiwa zaidi nchini.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza siku ya Jumatatu, Millicent Odhiambo alisema kwamba utalii wa ndani umepiga hatua katika kuiimarisha sekta ya utalii nchini.

“Utalii wa ndani ulisaidia katika kuimarisha sekta hii hasaa baada ya mataifa kama vile Uiengereza kuwapa raia wake tahadhari za kuzuru Kenya, pale taifa hili lilipokuwa limekumbwa na msukosuko wa kiusalama,” alisema Adhiambo.

Aliongeza kuwa kuna haja ya Wakenya kubadili mfumo wao wa miezi ya kawaida ya likizo ili kuiwezesha sekta ya utalii kuimarika bila kutegemea mataifa mengine.