Serikali imetakiwa kuchunguza kwa kina waliohusika katika mauwaji baada ya uchaguzi 2007 na kuwachukulia hatua wahusika.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kauli hii ilitolewa na seneta wa Mombasa Hassan Omar, aliongezea kuwa lazima haki ipatikane kwa waliothirika na visa vya baada ya uchaguzi.

Siku ya Jumatano, Omar alisitiza kuwa licha ya mahakama ya ICC kuwaachilia huru naibu rais William Ruto na mwanahabri Joshua Arap Sang, lazima kuna wahusika wakuu waliohusika na wanafaa kukabiliwa kisheria.

Aliongeza kuwa ipo haja ya waliohusika na mauaji wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 kuchukuliwa hatua za kisherai ili haki ipatikane pamoja na kufidiwa kwa waathiriwa wa ghasia hizo.

Akiongea katika hoteli moja jijini Mombasa, aliongeza kuwa serikali kwa ushirikiano na upinzani inafaa kuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa fidia inatolewa kwa waathiriwa.

Wakati huo huo alitaka pande zote kuzingatia kupiga vita suala la ufisadi, kukua kwa uchumi pamoja na uboreshaji wa miundo msingi ikizingatiwa hakuna tena joto la ICC.

Aliongeza kuwa suala la ICC lilichangia kuenea kwa hisia za kikabila katika nchi, pamoja na safari za kila mara za wabunge na viongozi tofauti kuelekea nchini Uholanzi wakati wa kuendelea kwa vikao hivyo.