Afisa wa Haki na Sheria katika Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika Francis Gamba ameitaka serikali kuu kuhakikisha kuwa swala la kuwalipa fidia waathiriwa wa ghasia za baada ya uchuguzi wa mwaka wa 2007/2008 linatekelezwa vyema.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatano, Gamba alisema kuwa kuna Wakenya wengi waliopitia mateso na hata wengine kufurushwa katika makaazi yao na hadi sasa bado hawajajua hatima yao.

Gamba ameitaka serikali kubuni jopo maalum litakalohakikisha kuwa kila Mkenya aliyeathirika na ghasia hizo anapata haki bila ya kubaguliwa kwa misingi ya kidini, kikabila wa hata kisiasa kutokana na kuwa wote ni Wakenya.

"Tunataka serikali kuhakikisha kuwa inabuni jopo maalum litakalofuatilia maswala ya kuwafidia waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007/08 ili wapate haki,” alisema Gamba.

Afisa huyo alisema kuwa iwapo serikali itatekeleza vyema swala hilo bila ya ubaguzi wowote, basi nia ya viongozi waliokabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya ICC kuwaomba Wakenya msamaha itapokelewa vyema na waathiriwa hao.