Chama cha walimu nchini Knut tawi la Mombasa kimeitaka serikali kuwalipa walimu na maafisa wa usalama walioisimamia mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE ya mwaka uliopita.

Share news tips with us here at Hivisasa

Katibu wa Knut tawi la Mombasa Dan Aloo amesema kuwa hatua hiyo ya serikali kukataa kuwalipa walimu na maafisa hao wa polisi kwa miezi sita sasa ni kuhujumu haki yao ya kikatiba.

Aloo amewataka maafisa wapya wa baraza la mtihani nchini KNEC, kuweka mikakati ya kulipwa kwa watumishi hao huku akiitaka serikali kukoma kuwanyanyasa wafanyikazi wake kwa kutowalipa kwa muda unaostahili.