Serikali kuu kupitia Wizara ya Elimu imewahakikishia wanafunzi kuwa itagharamia ada za mitihani ya kitaifa.
Akiongea katika siku ya mwisho ya mkutano wa walimu wakuu mjini Mombasa, Bwana Robert Masese aliyekuwa akiwalisha Waziri Fred Matiang'I alisema serikali imetenga shilingi bilioni 2.9 kufanikisha mradi huo wa kulipa ada za mitihani ya KCPE na KCSE.
Aidha, Bwana Masese aliwahimiza wakuu wa shule kuzingatia marufuku ya maombi kwa wanafunzi wa darasa la nane na kidato cha nne yaliyotangazwa na Waziri Matiang’i ili kuzuia wizi wa mtihani.
Masese pia aliwatahadharisha wakuu wa shule za upili dhidi ya kuwatoza wanafunzi karo zaidi kuliko kiasi kilichoidhinishwa katika mwongozo wa ada uliotolewa mwaka uliopita na serikali.
Alisema kuwa watakaopatikana na hatia hiyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Rais Uhuru Kenyatta pia aliwaonya walimu dhidi ya kufuja pesa zinazotengewa elimu ya bure.