Serikali kuu inalenga kufufua kiwanda cha nyama cha Kibarani mjini Mombasa ili kuboresha shughuli za kibiashara na kutoa ajira kwa vijana wa eneo la Pwani.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Katibu wa kudumu katika Wizara ya Mifugo Dkt Andrew Tuimur alisema kiwanda hicho kinahitaji kima cha shilingi milioni 700 ili kifufuliwe tena na kuboresha biashara hiyo.

Tuimur alisema kwamba mikakati tayari inaendelezwa na kiwanda hicho kitafufuliwa na kuwekwa mitambo ya kisasa itakayowawezesha wafugaji kunufaika moja kwa moja na mifugo wao, pindi wanapochinjwa katika kiwanda hicho.

“Tumetenga pesa za kutosha kufufua upya kiwanda cha nyama cha Kibara, Mombasa, kuhakikisha kuwa kinafikia kiwango cha kimataifa ili kutoa ajira kwa vijana,” alisema Tuimur.

Kiwanda hicho cha nyama cha Kibarani kilisambaratika kwa kile kilichotajwa kama usimamizi mbaya.