Serikali za kaunti zimetakiwa kuwapaandisha vyeo wanamahabara wa kisanyansi nchini kama njia mojawapo ya kusaidia kuboresha utendakazi wao.
Pendekezo hilo lilitolewa na mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha wanamahabara wa kisayansi nchini Michael Wanga.
Akizungumza siku ya Jumatatu jijini Mombasa, Wanga alisema kuwa chama hicho kinaendeleza mazungumzo na serikali za kaunti kuhakikisha kuwa wanachama wake wanapandishwa daraja kulingana na viwango vyao vya masomo.
Pendekezo hilo linajiri baada ya kushuhudiwa hali duni ya mazingira ya kikazi na matatatizo yanayowakabili wanasayansi hao wa mahabara nchini.
Haya yanajiri huku ulimwengu ukitarajiwa kuadhimisha siku ya mahabara ya kisayansi mnamo Aprili 15, ambapo sherehe ya kitaifa humu nchini zitaandaliwa mjini Kisumu.